Monday, August 30, 2010

UWANJA WA TAIFA WA MPIRA WA MIGUU

KIGOGO KUMEKUCHA

Bara bara ya kigogo inavyoonekana mara baada ya kutengenezwa.

Msongamano wa magari ktk barabara mbali mbali jijini Dar es Salaam umesababisha serikali kutengeneza barabara nyingine zinazounganisha sehemu mbalimbali hapa jijini.hivi majuzi nilipata bahati ya kupita barabara ya kigogo inayounganisha maeneo ya katikati ya mji na maeneo kama ubungo,Tabata na sehemu nyinginezo mbalimbali mtu anazoweza kwenda kupitia barabara za Morogoro na Mandela.
Bara bara ya kigogo imekuwa ukombozi kwa wakazi wa maeneo kama Ubungo,kimara,Tabata na Mbezi ambao wamekuwa wakipata tabu sana kupita barabara ya Morogoro kutokana na msongamano wa magari katika barabara hiyo.
Aidha barabara hiyo imekuwa faida kubwa kwa wakazi wa Kigogo,Luhanga na Mabibo ambao walikuwa wanateseka sana kutokana na ubovu wa barabara hivyo wamiliki wa magari kukataa kupeleka magari yao katika barabara hiyo  ambayo imekuwa kiungo muhimu kwa wakazi wa pembezoni wa jiji hili na sehemu za katikati ya mji.